Usiku wa manane (saa 9 hadi saa 10 alfajiri) ndio wagonjwa wengi mahututi hufariki
Usiku wa manane (saa 9 hadi saa 10 alfajiri) ndio wagonjwa wengi mahututi hufariki
Ni jambo la kushangaza na kuchanganya kidogo Kama si sana lakini wagonjwa mahututi wengi (sio wote) hufariki usiku wa manane
Natambua fika jana jioni kuna watu wengi tu, wamewaacha wapendwa wao hospital wakitegemea kuwaona leo asubuhi, wengine wakiagana nao kabisa lakini hawatawaona ama hawataonana nao tena wakiwa hai
Wahudumu wa vyumba ama wodi za mahututi wanalitambua vema hili ndio maana nyakati kama hizi huwapitia na kujaribu kuwaamsha
Kwa imani zetu hizi nje ya taaluma inaaminika kwamba ndio mida ya ziraili mtoa roho hupita kunyofoa roho za watu.... Lakini kitalaam ni kwamba huu ni muda ambao mwili huwa kwenye total relaxation usingizini bila bughudha yoyote hivyo kwa mtu mgonjwa aliyezidiwa anaweza moyo wake ukashindwa kusukuma damu hivyo kupelekea mapigo ya moyo kusimama na kusababisha kifo chake
Kuna kesi za namna hii zinatokea hata kwa wenye afya kamili, inaitwa vifo vya usingizini....ndio maana sipendi kabisa kulala kipindi hiki
Dunia ina vituko kuna watu ni waoga kufa kiasi kwamba inapofika usiku huogopa kabisa kulala ukizingatia kwamba waneshaambiwa story kama hizi ama zile za usingizi ni nusu kifo!!! Na ikitokea wamepitiwa na usingizi ama wakiamka asubuhi hujikagua kuona kama wako hai bado.... Between ukifa wala huwezi kujua kama umekufa .. ....... kuna wakati hata mimi napata hizi hisia mjue
- New
kwa ujumbe huu ndio maana wengi ikifika mida hii hawataki tena kulala.... Lakini pia naona sasa unaweza kupata tafsiri sahihi ya GOODNIGHT.... Nakutakia usiku mwema!!!
No comments:
Post a Comment