Nafasi 200 za Kazi- Tume ya Utumishi wa Mahakama
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI 200
Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa aya ya 112(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aidha, kwa mujibu wa Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Na. 4/2011, Tume ya Utumishi wa Mahakama mbali na kuwa na majukumu mengine inalo jukumu la kuajiri watumishi wa kada mbalimbali wa Mahakama.
Hivyo, Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia Watanzania wenye sifa zilizoainishwa hapo chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wako tayari kufanya kazi katika Ofisi za Mahakama ya Tanzania zilizoko katika Mikoa mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi. Nafasi hizo ni
Hakimu Mkazi Daraja la II – (TJS 2) nafasi 100,
Katibu Mahsusi Daraja la III – (TGS B) nafasi 20,
Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – (TGS B) nafasi 45,
Mpokezi – (TGS A) nafasi 1,
Dereva Daraja la II – (TGOS A) nafasi 10,
Mlinzi (TGOS A) nafasi 21 na
Afisa TEHAMA Daraja la II Nafasi 3 (TGS.E).
Mwisho wa kupokea barua za maombi hayo ni tarehe 04/09/2017 saa 9:30 Alasiri.
Barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji zikionyesha anwani sahihi
pamoja na namba ya simu na kuambatisha:-
Nakala za vyeti vya taaluma na vya kidato cha nne/sita vithibitishwe na Hakimu/Wakili anayetambuliwa na Serikali (True copies of the originals).
Aidha, inasisitizwa kwamba:-
1 Waombaji wawe na umri kati ya miaka 18 na 44
2 Waombaji wakazi toka maeneo husika na wenye sifa zilizoainishwa
katika tangazo hili, watafikiriwa kwanza na kupangiwa kazi katika
maeneo husika.
3 Maombi yote yapitishwe kwa Katibu Tawala wa wilaya anayoishi
mwombaji.
4 Waombaji walio katika Utumishi wa Umma wapitishe maombi yao kwa
waajiri wao wa sasa.
5 Waombaji walioacha kazi katika Utumishi wa Umma waeleze kwamba
waliacha kazi Serikalini na sababu ya kufanya hivyo.
6 Waombaji watakao shinda usaili na kuajiriwa watakuwa watumishi wa
Mahakama ya Tanzania.
7 Waombaji waliosoma nje ya nchi vyeti vyao vithibitishwe na TCU/NACTE.
8 Waombaji waandike majina yao yote matatu kwa kirefu.
9 Waombaji waandike nafasi ya kazi wanayoomba nyuma ya bahasha
watakazotumia maombi yao.
10 Waombaji wasiwe walioachishwa/kufukuzwa kazi kwenye Utumishi wa
Umma.
11 Mwombaji asiandike barua zaidi ya moja kwa ajili ya kuomba nafasi
moja.
12 Waombaji wote wasio na sifa zilizotajwa na ambao hawatazingatia
mojawapo ya masharti yaliyotajwa hapo juu, maombi yao
hayatashughulikiwa.
Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kwa Katibu, Tume ya Utumishi
wa Mahakama ya Tanzania, S.L.P. 8391 , DAR ES SALAAM.
Imetolewa na ;-
Katibu,
Tume ya Utumishi wa Mahakama,
S.L.P 8391,
DAR ES SALAAM.
Source NAFASI 200 ZA KAZI- TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA
Hivyo, Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia Watanzania wenye sifa zilizoainishwa hapo chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wako tayari kufanya kazi katika Ofisi za Mahakama ya Tanzania zilizoko katika Mikoa mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi. Nafasi hizo ni
Hakimu Mkazi Daraja la II – (TJS 2) nafasi 100,
Katibu Mahsusi Daraja la III – (TGS B) nafasi 20,
Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – (TGS B) nafasi 45,
Mpokezi – (TGS A) nafasi 1,
Dereva Daraja la II – (TGOS A) nafasi 10,
Mlinzi (TGOS A) nafasi 21 na
Afisa TEHAMA Daraja la II Nafasi 3 (TGS.E).
Mwisho wa kupokea barua za maombi hayo ni tarehe 04/09/2017 saa 9:30 Alasiri.
Barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji zikionyesha anwani sahihi
pamoja na namba ya simu na kuambatisha:-
- Vivuli vya vyeti vyote vya elimu na mafunzo.
- Ufupisho wa taarifa za mwombaji (CV).
- Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
- Picha mbili za rangi (Passport size) zilizopigwa hivi karibuni.
Aidha, inasisitizwa kwamba:-
1 Waombaji wawe na umri kati ya miaka 18 na 44
2 Waombaji wakazi toka maeneo husika na wenye sifa zilizoainishwa
katika tangazo hili, watafikiriwa kwanza na kupangiwa kazi katika
maeneo husika.
3 Maombi yote yapitishwe kwa Katibu Tawala wa wilaya anayoishi
mwombaji.
4 Waombaji walio katika Utumishi wa Umma wapitishe maombi yao kwa
waajiri wao wa sasa.
5 Waombaji walioacha kazi katika Utumishi wa Umma waeleze kwamba
waliacha kazi Serikalini na sababu ya kufanya hivyo.
6 Waombaji watakao shinda usaili na kuajiriwa watakuwa watumishi wa
Mahakama ya Tanzania.
7 Waombaji waliosoma nje ya nchi vyeti vyao vithibitishwe na TCU/NACTE.
8 Waombaji waandike majina yao yote matatu kwa kirefu.
9 Waombaji waandike nafasi ya kazi wanayoomba nyuma ya bahasha
watakazotumia maombi yao.
10 Waombaji wasiwe walioachishwa/kufukuzwa kazi kwenye Utumishi wa
Umma.
11 Mwombaji asiandike barua zaidi ya moja kwa ajili ya kuomba nafasi
moja.
12 Waombaji wote wasio na sifa zilizotajwa na ambao hawatazingatia
mojawapo ya masharti yaliyotajwa hapo juu, maombi yao
hayatashughulikiwa.
Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kwa Katibu, Tume ya Utumishi
wa Mahakama ya Tanzania, S.L.P. 8391 , DAR ES SALAAM.
Imetolewa na ;-
Katibu,
Tume ya Utumishi wa Mahakama,
S.L.P 8391,
DAR ES SALAAM.
Source NAFASI 200 ZA KAZI- TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA
No comments:
Post a Comment