[TRENDING][10]

CENTER OF ICT
ENTERTAINMENT
GOSSIP
NEWZ
SPORTS
VIDEOS

WAZIRI ALIYEUAWA AZIKWA SOMALIA.

Abbas hakuwa na uzoefu mkubwa katika siasa lakini alipendwa na wengi
Image captionAbbas hakuwa na uzoefu mkubwa katika siasa lakini alipendwa na wengi
Waziri wa ujenzi nchini Somalia aliyeuawa na na mwanajeshi wa serikali mjini Mogadishu siku ya Jumatano Abbas Abdullahi Siraji amezikwa katika mazishi ya kitaifa.
Mmoja wa wanajeshi wa serikali alifyatua risasi katika gari la waziri huyo alipokua akikaribia ikulu ya Rais.
Maafisa wa usalama wanasema kuwa mlinzi huyo alidhani gari hilo lingeleta madhara kiusalama na hakujua kuwa lilikuwa la waziri huyo.
Rais Mohammed Abdullahi Farmajo ameamuru kufanyika kwa uchunguzi wa kina.
Ameahirisha pia safari yake ya kikazi nchini Ethiopia kwa ajili ya kuhudhuria mazishi hayo.
Abbas alikua mkimbizi katika kambi ya Dadaab na baadae kuwa waziri mdogo zaidi nchini humo huku akihamasiaha raia wengi wa nchi hiyo.

About Author Mohamed Abu 'l-Gharaniq

when an unknown printer took a galley of type and scrambled it to make a type specimen book. It has survived not only five centuries.

No comments:

Post a Comment

Start typing and press Enter to search