SPORTPESA YAFIKIA PATAMU
Timu ya Gor Mahia yatinga nusu fainali SportPesa
Gor Mahia imekuwa timu ya pili ya Kenya kutinga nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup.
AFC
Leopards ndiyo timu ya kwanza ya Kenya kufuzu nusu fainali baada ya
kuishinda Singida United na itacheza na Yanga hatua ya nusu fainali.Gor Mahia imefuzu baada ya kuitwanga Jang'ombe Boys ya Zanzibar kwa mabao 2-0 katika mchezo wa robo fainali uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar.
Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere ndiye mfungaji wa mabao yote mawili katika dakika ya 66 na 78. Sasa Gor Mahia wanasubiri mshindi kati ya Simba dhidi ya Nakuru All Stars ya Kenya pia ambao umeanza tayari.
No comments:
Post a Comment