[TRENDING][10]

CENTER OF ICT
ENTERTAINMENT
GOSSIP
NEWZ
SPORTS
VIDEOS

Kylie Jenner and David Beckham wanapata pesa nyingi kupitia Instagram

Kylie Jenner and David Beckham wanapata pesa nyingi kupitia Instagram

Nyota wa vipindi vya Telesheni Kylie Jenner ametajwa kuwa ni mwanadada anayepata pesa nyingi, kutokana na ukurasa wake wa Instagram huku David Beckham akiongoza
Kipindi cha Televisheni cha The Keeping Up with the Kardashians kinakadiriwa kuingiza dola milioni moja kwa tangazo moja la wadhamini.
Beckham, 43,ameripotiwa kulipisha mpaka dola za Marekani laki tatu kwa kila chapa.
Mwanamitindo na mama wa mtoto mmoja alimpiku mshindi wa mwaka 2017 Selena Gomez, ambaye ameshika nafasi ya pili,Dada yake, Kim Kardashian West ameshika nafasi ya nne.
Waimbaji Beyonce na Justine Bieber, muigizaji Dwayne Johnson na nyota wa mpira wa miguu Neymar na Cristiano Ronaldo wameshika nafasi kumi za mwanzo.
Data zinatoka kwenye kampuni ya Hopper HQ, ambayo inaendesha anuani za mitandao ya kijamii kwa niamba ya makampuni na watu binafsi.Kampuni hiyo ilichapisha orodha ya kwanza ya instagram kuhusu watu matajiri mwaka jana.
Orodha hii na gharama kwa kila posti imepatikana baada ya kuzungumza na wanaoitwa ''washawishi'' wenyewe, sambamba na makampuni yanayohusika na masuala ya chapa na masoko, kwa ajili ya kukadiria kiasi gani kila akaunti inatoza
Hata hivyo makampuni hayo hufanya siri kuhusu malipo , au posti hivyo kiasi cha malipo hasa yanayofanyika hakijulikani.
Jenner mwenye miaka 20 ana wafuasi milioni 111 kwenye akaunti yake ya Instagram, anatazamiwa kuwa bilionea mdogo kuwahi kutokea.
Ni kutokana na vipodozi vyake, Kylie Cosmetics, vimesaidia kumfikisha kwenye mafanikio hayo mwaka 2018 baada ya kushika nafasi ya nne mwaka jana.
Wanafamilia wengine wa Kardashian ni Kendall Jenner na Khloe Kardashian, wameshika nafasi ya 10 na 11 mtawalia.
David Beckham is ameorodheshwa wa 12 duniani. Posti zake za hivi karibuni zilionesha akitangaza saa chapa ya Tudor na Adidas.
Anayemfuatia kwa kundi la waingereza wanaolipwa vizuri ni Gareth Bale,ambaye posti zake zina thamani ya dola 185,000
fedha hizo zimeongezeka kwa kiasi kikubwa tangu mwaka jana.Mwaka 2017,mshawishi wa juu kabisa alikadiriwa kupata mpaka dola 550,000 kwa kila posti moja ya Instagram, ukilinganisha na dola milioni moja mwaka huu.
Mike Bandar , mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Hopper HQ amesema ongezeko hili linatokana na jitihada zilizowekwa na makampuni ya masoko, kuondoka kwenye mfumo wa matangazo kupitia Televisheni na machapisho na wameshuhudia kupata faida kubwa katika uwekezaji wao kupitia mitandao ya kijamii.

Nyota wanaoingiza pesa nyingi

1. Kylie Jenner: wafuasi milioni 111 anapatta $1m (£760,000) kwa kila posti
2. Selena Gomez: ana wafuasi milioni 139 anapata $800,000 kwa kila posti
3. Cristiano Ronaldo ana wafuasi milioni 137 anapata $750,000 kwa kila posti
4. Kim Kardashian West ana wafuasi milioni 114 hupata $720,000 kwa kila posti
5. Beyonce Knowles ana wafuasi milioni 116 hupata $700,000 kwa posti moja
6. Dwayne Johnson ana wafuasi milioni 111 hupata $650,000 kwa posti moja
7. Justin Bieber ana wafuasi milioni 101 hupata $630,000 kwa kila posti
8. Neymar da Silva Santos Junior ana wafuasi milioni 100,hupata $600,000 kwa kila posti moja
9. Lionel Messi ana wafuasi milioni 97, hupata $500,000 kwa posti moja
10. Kendall Jenner ana wafuasi milioni 93, hupata $500,000 kwa kila posti

Nyota watano waingereza wanaopata fedha nyingi

1. David Beckham ana wafuasi milioni 49 huingiza $300,000 kwa posti
2. Gareth Bale ana wafuasi milioni 35 hupata $185,000 kwa posti moja
3. Zoe Sugg ana wafuasi milioni 10, hupata $16,000 kwa posti moja
4. Rosie Huntington-Whiteley ana wafuasi milioni 8 hupata $11,500
5. Jamie Oliver ana wafuasi milioni 6, huingiza $8,000 kwa posti moja

About Author Mohamed Abu 'l-Gharaniq

when an unknown printer took a galley of type and scrambled it to make a type specimen book. It has survived not only five centuries.

No comments:

Post a Comment

Start typing and press Enter to search