[TRENDING][10]

CENTER OF ICT
ENTERTAINMENT
GOSSIP
NEWZ
SPORTS
VIDEOS

Bomu la Vita Vikuu vya Dunia lateguliwa Frankfurt, Ujerumani

Bomu la Vita Vikuu vya Dunia lateguliwa Frankfurt, Ujerumani


Wataalamu wa kutegua mabomu wa Ujerumani wakiwa wameketi karibu na bomu hilo Jumapili (03 September 2017)

Wataalamu wa kutegua mabomu mjini Frankfurt, Ujerumani siku ya Jumapili walifanikiwa kutegua bomu kubwa ambalo halikuwa limelipuka ambalo liliangushwa wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Bomu hilo la tani 1.4 kutoka Uingereza liligunduliwa katika eneo la ujenzi Jumatano.
Habari hizo zilipokelewa kwa shangwe na watu zaidi ya 65,000 ambao walikuwa wamehamishwa maeneo yao kwa sababu za kiusalama baada ya bomu hilo kuteguliwa.
Hiyo ilikuwa idadi kubwa zaidi ya watu kuhamishwa tangu kutokea kwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia nchini Ujerumani, na shughuli hiyo ilihusisha mamia ya maafisa wa serikali.
Maeneo ambayo watu walihamishwa yalikuwa katika mtaa wa Westend, na ni pamoja na hospitali kadha, nyumba za kuwatunza wagonjwa na hata katika Benki Kuu ya Ujerumani.
Inaaminika kwamba kuna mamia ya maelfu ya mabomu ya wakati wa vita ambayo hayakulipuliwa ambayo yametapakaa kote Ujerumani.
BomuHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBomu hilo la tani 1.4 kutoka Uingereza lilipatikana katika eneo la ujenzi Jumatano
Frankfurt (03 September 2017)Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWatu waliohamishwa wanatarajiwa kuruhusiwa kurejea makwao karibuni
Frankfurt (03 September 2017)Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBarabara zilifungwa na maafisa wa polisi Jumapili asubuhi
Polisi wakitumia helikopta na kamera za kupima viwango vya jotoHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionPolisi wakitumia helikopta na kamera za kupima viwango vya joto walipaa angani eneo hilo wataalamu wa kutegua bomu walipokuwa wakiendelea na kazi yao

About Author Mohamed Abu 'l-Gharaniq

when an unknown printer took a galley of type and scrambled it to make a type specimen book. It has survived not only five centuries.

No comments:

Post a Comment

Start typing and press Enter to search