[TRENDING][10]

CENTER OF ICT
ENTERTAINMENT
GOSSIP
NEWZ
SPORTS
VIDEOS

Wazungu waliomlazimisha mtu mweusi kuingia katika jeneza hatiani

Wazungu waliomlazimisha mtu mweusi kuingia katika jeneza hatiani


Wakulima wazungu ,Theo Martins Jackson na mwenzake Willem Oosthuizen

Wakulima wawili wazungu nchini Afrika Kusini waliomlazimisha mtu mweusi kuingia katika jeneza wamepatikana na hatia ya jaribio la mauaji na utekaji nyara.
Victor Mlotshwa mwenye umri wa miaka 27 alipigwa na kulazimishwa kuingia katika jeneza na wawili hao Theo Martins Jackson na mwenzake Willem Oosthuizen mwaka 2016.
Wawili hao bado hawajahukumiwa. Walikuwa wamekana mashataka hayo.
Kesi hiyo ilizuia hisia kali nchini Afrika Kusini na kuangazia wasiwasi wa ubaguzi wa rangi miongoni mwa wakulima .
Bwana Mlotshwa aliripoti kisa hicho baada ya kanda ya video ya unyanyasaji huo kuonekana katika mtandao wa YouTube miezi kadhaa baadaye.
Katika hati ya kiapo ya mahakamani Jackson na Oosthuizen walisema hawakulenga kumuumiza bwana Mlotshwa lakini walitaka kumpatia funzo.
Victor Mlotshwa mwenye umri wa miaka 27 alipigwa na kulazimishwa kuingia katika jeneza
Image captionVictor Mlotshwa mwenye umri wa miaka 27 alipigwa na kulazimishwa kuingia katika jeneza
Huku Jaji Segopojte akitoa uamuzi wake katika mahakama ya Middelburg siku ya Ijumaa, wafuasi wa mwathiriwa huyo walisherehekea.
''Nafurahi kwamba hatimaye haki imepatikana'' , bwana Mlotshwa aliambia BBC.

About Author Mohamed Abu 'l-Gharaniq

when an unknown printer took a galley of type and scrambled it to make a type specimen book. It has survived not only five centuries.

No comments:

Post a Comment

Start typing and press Enter to search