[TRENDING][10]

CENTER OF ICT
ENTERTAINMENT
GOSSIP
NEWZ
SPORTS
VIDEOS

Watu 13 wafariki katika makabiliano na polisi India

Watu 13 wafariki katika makabiliano na polisi India


Magari kadhaa yameteketezwa moto huko Panchkula

Yamkini watu 13 wameuwawa kaskazini mwa India, baada ya ghasia kutokea, mara baada ya mahakama moja nchini humo, kumhukumu Guru mmoja anyemiliki dhehebu lake na anayejiita mtu mzuri, kwa kosa la kuwabaka wanawake.
Idara ya polisi inasema kuwa baadhi ya waumini wa mtu huyo wanaodaiwa kufikia milioni moja, walianzisha ghasia ya kuwarushia polisi kila aina ya silaha ikiwemo mawe, mara tu mahakama ilipotoa hukumu hiyo.
Umati wa watu ukiharibu gari la Televisheni, baada ya mahakama kutoa hukumu hiyo huko PanchkulaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionUmati wa watu ukiharibu gari la Televisheni, baada ya mahakama kutoa hukumu hiyo huko Panchkula
Duru kutoka mji wa Panchkula zinathibitisha kuwa watu hao 13 kweli wamefariki, huku wawili wakiwa katika hali mahututi.
Gurmeet Ram Rahim Singh anasemekana kuwa na waumini wanaofikia milioni moja, India
Image captionGurmeet Ram Rahim Singh anasemekana kuwa na waumini wanaofikia milioni moja, India
Hii ni kwa mjibu wa taarifa kutoka makao makuu ya Polisi katika jimbo la Panchkula, kaskazini mwa India.
Awali kulikuwa na hofu ya kutokea fujo, baada ya kiongozi huyo wa kidini:- Gurmeet Ram Rahim Singh, alipopatikana na hatia ya kuwanyanyasa kingono waumini wake wawili wa kike, katika kesi hiyo ya mwaka 2002.
Makumi kwa maelfu ya wafuasi wa Guru huyo wakimiminika mjini ChandigarhHaki miliki ya pichaMANOJ DHAKA
Image captionMakumi kwa maelfu ya wafuasi wa Guru huyo wakimiminika mjini Chandigarh
Kisa hicho kinadaiwa kufanyika katika makao makuu ya kiongozi wa kundi hilo la Dera Sacha Sauda, iliyoko katika mji wa Sirsa, Kaskazini mwa India.
Ramani ya India
Image captionRamani ya India

About Author Mohamed Abu 'l-Gharaniq

when an unknown printer took a galley of type and scrambled it to make a type specimen book. It has survived not only five centuries.

No comments:

Post a Comment

Start typing and press Enter to search