[TRENDING][10]

CENTER OF ICT
ENTERTAINMENT
GOSSIP
NEWZ
SPORTS
VIDEOS

usajili kumi bora uliokamilika kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu mwishoni mwa mwezi Agosti

  usajili kumi bora uliokamilika kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu mwishoni mwa mwezi Agosti.

Dirisha la usajili linatarajiwa kufungwa mwishoni mwa mwezi wa saba kabla ya pazia la Ligi Kuu Bara alijafunguliwa mwezi wa nane kwa klabu zote kuanza kulisaka taji hilo
Klabu zote 16 zipo kwenye maandalizi makubwa ya kuboresha vikosi vyao kwa kuongeza wachezaji ambao watakuja kuwa na msaada ndani ya timu 
Singida United imewashangaza wengi katika kipindi hiki cha usajili kwa kufanya kufuru kwa kumwaga pesa kuliko hata klabu kubwa hapa nchini kama Simba, Azam na Yanga.

  usajili kumi bora uliokamilika kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu mwishoni mwa mwezi Agosti.

10.Ditram Nchimbi (Njombe Mji)
Mshambuliaji mpya wa klabu ya Njombe mji akitokea klabu ya Mbeya City aliyeitumikia msimu uliopita, uzoefu wake kwenye Ligi na umairi wake utakuwa msaada kwa timu yake hiyo mpya
9.Youthe Rostand (Yanga)
Mmoja wa walinda mlango bora kwa msimu uliopita, Rostand amejiunga na Yanga akitokea klabu ya African Lyon iliyoshuka daraja
8.Bakari Masoud (Mbeya City)
Bakari Masoud amewahi kuchezea Coastal Union, Yanga SC, Fanja FC (Oman), PDRM FC (Malaysia), African Sports na Free State ya Afrika Kusini kabla ajasaini Mbeya City kwa msimu ujao
7.Said Kipao (Kagera Sugar)
Ukitaja walinda mlango bora chipukizi kwa msimu ulioisha jina la Said Kipao litakuwa miongoni mwao, ni usajili bora kwa Kagera Sugar ukizingatia ubora na umri mdogo wa mlinda mlango huyo
6.Salum Mbonde (Simba)
Mlinzi wa zamani wa Mtibwa Sugar na timu ya taifa stars, amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili, ni moja wa usajili bora kwa Mnyama katika idara ya safu ya ulinzi
5.Wazir Junior (Azam)
Baada ya kuwa na wakati mzuri ndani ya TOTO Africa, Azam wamefanikiwa kuinasa saini ya mshambuliiaji huyo mwenye uwezo wa juu na nguvu za kupambana na mabeki 
4.Ibrahim Ajibu (Yanga)
Ni usajili utakao kuwa na faida ndani ya Yanga kwa msimu ujao, Ajibu ataleta faida kubwa ndani ya timu kwani ana uwezo mkubwa wa kufunga magoli kadhalika na kutoa pasi za mwisho
3.Emmanuel Okwi (Simba)
Ametokea klabu ya Villa ya nchini Uganda kabla ya kujiunga na Mnyama, Okwi atakuja kuifanya Simba kuwa tishio kwa msimu ujao kwani ana ifahamu vyema Ligi Kuu 
2.Mbaraka Yusuph (Azam)
Ametokea Kagera na kujiunga na Waoka mikate kuja kurithi namba ya John Boco aliyejiunga na Simba, Mbaraka ni mmoja wa wafungaji bora wazawa kwa sasa kwa misimu miwili ndani ya Kagera ameonesha ubora wake
1.Dany Usengimana (Singida United)
Mfungaji bora wa Ligi kuu Rwanda kwa misimu miwili mfululizo na Striker wa timu ya Taifa ya Rwanda ametua Singida United kwa kandarasi ya miaka miwili.

About Author Mohamed Abu 'l-Gharaniq

when an unknown printer took a galley of type and scrambled it to make a type specimen book. It has survived not only five centuries.

No comments:

Post a Comment

Start typing and press Enter to search