Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 21.07.2017
Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 21.07.2017 .
Dau la Manchester City la pauni milioni 44.5 la kumtaka beki wa kushoto wa Monaco, Benjamin Mendy, 23, limekataliwa. Monaco wanataka pauni milioni 54. (Daily Mail)
Manchester City wapo tayari kumfanya Benjamin Mendy, 23, kuwa beki ghali zaidi duniani kwa kumsajili kutoka Monaco. (L'Equipe)
Manchester City watakamilisha usajili wa Danilo, 26, kutoka Real Madrid siku ya Ijumaa. (Marca)
Beki wa Manchester City Aleksander Kolarov anakaribia kujiunga na Roma, kwa mujibu wa meneja wake Pep Guardiola. (Sky)
Barcelona wamewasilisha dau la pauni milioni 72 kumtaka kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, lakini Liverpool wanatarajiwa kutupilia mbali dau hilo. (Daily Mail)
Liverpool wamesema Barcelona wanapoteza muda wao kutaka kumsajili Philippe Coutinho, 25. (Liverpool Echo)
Juventus wanataka kuimarisha kiungo chao kwa kumsajili Emre Can kutoka Liverpool. (Gianluca Dimarzio)
Arsenal wana uhakika kuwa kiungo wao Mesut Ozil, 28, atasaini mkataba mpya kubakia Emirates. (Sun)
Manchester United sasa wameelekeza nguvu zao kumtaka beki wa kulia wa Paris Saint-Germain, Serge Aurier, 24, kutokana na kusuasua kwa mipango ya kumsajili Fabinho, 23, kutoka Monaco. (Independent)
Meneja wa PSG Unai Emery amethibitisha kuwa Serge Aurier anataka kuondoka Paris msimu huu. (L'Equipe)
Manchester United wanataka kuwazidi kete AC Milan katika kumsajili Renato Sanches kutoka Bayern Munich. (The Guardian)
Manchester United bado hawajafikia dau wanalotaka Inter Milan katika kumsajili Ivan Perisic, 28. (Daily Mirror)
Jose Mourinho ameitaka klabu yake ya Manchester United kumsaidia kusajili mchezaji mmoja tu zaidi "haraka iwezekanavyo". (Sky Sports)
Wolfsburg wameulizia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial. (Kicker)
Diego Costa huenda akacheza kwa mkopo AC Milan, wakati akisubiri kuhamia Atletico Madrid. (Don Balon)
Chelsea wapo tayari kumuuza Diego Costa kwenda Atletico Madrid kwa pauni milioni 44, na sio pauni milioni 25 zilizotolewa na Atletico. (Independent)
Alexis Sanchez, 28, amefikia makubaliano na Paris Saint-Germain, na klabu hiyo ya Ufaransa itapanda dau la pauni milioni 45. Kinachosubiriwa ni kauli ya Arsene Wenger. (Sun)
Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere, 25, yuko tayari kwenda West Ham, iwapo klabu hiyo itafikia makubaliano kuhusu ada ya uhamisho. (Daily Star)
Arsenal wamekataa dau la pauni milioni 16, la kumsajili beki wake Callum Chambers. Arsenal wanataka pauni milioni 20. (Daily Telegraph)
Tottenham wametaka kufahamishwa msimamo wa Riyad Mahrez, lakini Leicester watalazimika kupunguza bei ya pauni milioni 50, kama watamuuza kwenda White Hart Lane. (Standard)
Wachezaji wa Leicester City wapo tayari 'kumhamasisha kwa lazima' Riyad Mahrez ikiwa hatajituma kwa asilimia 100, amesema kiungo Andy King. (Leicester Mercury)
Meneja wa Leicester City Craig Shakespeare amethibitisha kuwa wamekataa dau kutoka Roma la kumtaka Riyad Mahrez. (Sky Transfer Centre)
Arsenal na Tottenham zinamnyatia winga kinda wa Manchester City Jadon Sancho, 17. (Independent)
Mshambuliaji wa Stoke City, Marco Arnautovic, 28, atakuwa mchezaji anayelipwa zaidi West Ham baada ya kukamilisha vipimo vyake vya afya siku ya Ijumaa. (Daily Express)
- Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 17.07.2017
- Arsenal wana wasiwasi kuhusu kuuziwa Lemar
- West Ham wakaribia kumchukua Chicarito
Torino wanataka AC Milan itoe euro milioni 50 pamoja na M'Baye Niang, Gabriel Paletta na Manuel Locatelli, kama wanamtaka Andrea Belotti. (La Stampa)
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii (Kwa Kiingereza): Uhamisho wa wachezaji Ulay
No comments:
Post a Comment