WAGOMBEA WAWILI WAEKEWA PINGAMIZI UCHAGUZI WA TFF
Dar es Salaam. Wagombe wa nafasi mbalimbali za
uongozi katika uchaguzi wa Shirikisho la Soka (TFF), wamefika asubuhi
kwa ajili ya usaili huku wawili kati 73 wakiwekewa pingamizi.
Waliowekewa
pingamizi ni Wales Kiria ambaye amewekewa pingamizi na John Kijumbe,
Mussa Sima na amewekewa pingamizi na Hussen Mwamba.
Mwenyekiti
wa Kamayi ya Uchaguzi, Revocatus Kuuli alisema kuwa kabla ya kuanza
usaili saa 6 kamili mchana wataanza kwa kusikiliza pingamizi hizo na
baada ya kutoa majibu wataanza usaili.
"Tunaanza kwanza
kusikiliza hizi pingamizi na kuzitolea majibu na halafu saa 6, kamili
mchana ndio usaili utaanza kutokana na majina ya wagombea waliowahi
kufika na kuandika jina mapema kwenye karatasi ya waliofika hapa leo,"
alisema Kuuli.
Kuuli alisema pia kwa wale wagombea
ambao hawapo siku ya leo siku bado hazijaisha zimebaki siku mbili
kwahiyo hata kama watakuwa na mapingamizi nao watawasikiliza pia.
No comments:
Post a Comment