Maneno ya Vanessa Mdee baada ya Jux kupost picha za Graduation
Maneno ya Vanessa Mdee baada ya Jux kupost picha za Graduation
June 22, 2017 baada ya maswali ya watu mbali waliokuwa wanahoji kitu alichokuwa anafanya Jux China hatimaye mwimbaji huyo staa wa Bongofleva ameonesha picha za graduation ya kuhitimu Degree ya Computer Science kutoka Guangdong University.Jux kuonesha picha hizo kupitia Instagram yake kumewafanya watu wengi watoe pongezi kwake ambapo miongoni mwao ni Vanessa Mdee ambaye ametumia ukurasa wake wa Instagram pia kuelezea hisia zake.
“Congratulation Juma jux U finally done and you done did it well. Hapo watu walikuwa wakiombaga picha za wewe darasani nadhani hii picha jibu la kutosha. Umeweza kufanya yote, MZIKI, BIASHARA NA SHULE… now that’s exceptional. Muda wa vibunda babaaa. Keep inspiring the YUTEEEEE” – Vanessa Mdee.