Kaburu na Aveva Ndani mpaka July 13 – Haya hapa makosa yao 5
Kaburu na Aveva Ndani mpaka July 13 – Haya hapa makosa yao 5
Washitakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kutakatisha fedha ambayo ni dola za Marekani 300,000 walizozipata kwa kughushi nyaraka kuonesha kwamba Club ya Simba imelipa deni la fedha hiyo kwa Aveva.
Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alisema mashitaka hayana dhamana hivyo aliahirisha hadi Julai 13 mwaka huu kujua hatua ya upelelezi umefikia wapi.
MAKOSA 5 YALIYOTAJWA KWENYE KESI
Makosa 5 yanayowakabili Rais wa Simba Aveva na makamu wake Kaburu
1. Kughushi
Aveva alighushi nyaraka ili kujilipa deni ambalo inadaiwa aliikopesha Simba USD 300,000.
2. Nyaraka za uongo
Walitumia nyaraka za uongo ili kulipa deni kutoka benki ya CRDB.
3. Kutakatisha fedha
Tarehe tofauti Aveva na Kaburu walikula njama za kutakatisha fedha UDS 300000.
4. Kutakatisha fedha
Aveva alijipatia fedha kutoka Barclays bank tawi la Mikocheni.
5. Kutakatisha fedha Kaburu
Kaburu alimsaidia Aveva kupata pesa USD 300,000 kutoka Barclays Bank tawi la Mikocheni.
No comments:
Post a Comment