[TRENDING][10]

CENTER OF ICT
ENTERTAINMENT
GOSSIP
NEWZ
SPORTS
VIDEOS

Jakarta, mji unaozama kwa kasi ya juu zaidi duniani

Jakarta, mji unaozama kwa kasi ya juu zaidi duniani.


Mji mkuu wa Indonesia Jakarta ni nyumbani kwa watu milioni 10 lakini mji huo pia unazama kwa kasi zaidi duniani. Ikiwa hatua hazitachukuliwa sehemu za mji huo mkubwa huenda zikazama kabisa ifikapo mwaka 2050 kwa mujibu wa watafiti.
Mji huo uko eneo lenye kinamasi kando mwa bahari, huku mito 13 ikipita kwenye mji huo na hivyo sio jambo la kushangaza kuwa mafuriko ni jambo la kawaida mjini Jakarta kwa mujibu wa wataalamu, hali inayozidi kuwa mbaya na mji huo ukizidi kutoweka.
"Uwezekano wa Jakarta kuzama sio jambo la kufanyiwa mzaha," anasema Heri Andreas, ambaye amechuguza kutokewa kwa ardhi kwenda mjini Jakarta kwa miaka 20.
"Tukiangangalia uchunguzi wetu ifikapo mwaka 2050 karibu asilimia 95 ya eneo la Kaskazini mwa Jakarta litakuwa limezama.
Picture of a dike in North Jakarta.
Image captionHeri Andreas anaonyesha ukuta uliojengwa kuzuia maji ya bahari kufurika nyumba
Tayari inafanyika - eneo la Kaskazini mwa Jakarta limezama mita 2.5 katika kipindi cha 10 na linazidi kuzama kwa karibu sintimita 25 kwa mwaka sehemu zingine.
Jakarta huzama kwa kasi ya sentimita 1-15 kwa mwaka na karibu nusu ya mji uko chini ya bahari.
Athari tayari zimeonekana Kaskazini mwa Jakarta.
Kwenye wilaya ya Muara Baru, jengo lote la ofisi limebaki mahame. Awali ilikuwa ni kampuni ya uvuvi lakini ghorofa ya kwanza ndiyo tu inaweza kutumiwa.
Picture of a sunken building.
Image captionSehemu ya kwanza ya jengo sasa iko ardhini
Sehemu ya kwazza sasa imebaki kufurika maji. Ardhi inayozunguka iko juu kwa hivyo maji hayawezi kutoka.
Picture of a flooded ground floor of the abandoned building.
Image captionMaji yaliyokwama chumba cha chini
Mwaka baada ya mwingine ardhi imekuwa ikizama.
Eneo la Kaskazini mwa Jakarta lina historia ya bandari na hata sasa ndiyo ilipo bandari yenye shughuli nyingi zaidi chini Indonesia, Tanjung Priok.
Leo hii watu 1.8 wanaishi eneo hilo.
Fortuna Sophia anaishi kwenye nyumba ya kifahari, Kuzama kwa nyumba yake hakuwezi kuonekana mara moja lakini anasema nyufa huonekana kwenye kuta na nguzo kila baada ya miezi sita.
Fortuna
Image captionFortuna
Ameishi hapa kwa miaka minne lakini eneo hjlo mara kadhaa limefurika: " Maji ya bahari huinga na kufurika kabisa kidimbwi cha kuogelea. Inatubidi tuhamishe kila kitu kwenda ghorofa ya kwanza." anasema
Athari kwa nyumba ndogo karibu na bahari zinaonekana. Wakaazi ambao wakati mmoja walikuwa wanaiona bahari kwa sasa wanaona ukuta uliojengwa kuzuia maji ya bahari.
"Kila mwaka maji ya bahari hupanda sentimita 5," mvuvi Mahardi anasema.
Map of Indonesia and Jakarta
Image captionRamani ya Indonesia na Jakarta
Maeneo mengine ya Jakarta nayo yanazama kwa mwendo wa chini. Magharibi mwa Jakarta, ardhi inazama kwa karibu sentimita 15 kwa mwaka, kwa sentimita 10 mashariki, sentimita 2 kati kati mwa Jakarta na sentimita 1 kusini mwa Jakarta.
Miji iliyo pwani kote duniani imeathiriwa kutokana na kupanda kwa viwango vya bahari kufuatia na mabadiliko ya hali ya hewa, Kuongezeka kwa viwango vya bahari husababisha kuongezeka kwa joto na kuyeyuka kwa theluji. Kasi ya kuzama kwa mji wa Jakarta imewatia wasiwasi wanasayansi.
Kuzama kwa mji wa Jakarta kumetokana na kutumika kwa maji wa chini ya ardhi kupitia uchimbaji visima kwa kunywa, kuoga na matumizi mengine ya kila siku miongoni mwa wakaazi wa mji.
Maji ya mifereji hayapatikani sehemu zingine kwa hivyo watu hawana lingine ila kutafuta maji mbali zaidi chini ya ardhi.
Picture of a water pump.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionWengi wa wakaazi wa Jakarta hutegemea maji ya visima
Hendri, mmiliki mmoja wa nyumba huko Jakarta ana jumba la makaazi linalofahamika kama kos-kosan na amekuwa akitumia maji ya kisima kwa miaka 10 kwa wapangaji wake. Ni mmoja kati ya wamiliki wengi ya nyumba wanaofanya hivyo.
"Ni vizuri tutumie maji yetu kuliko kutegemea mamlaka . kos kosan uhitaji maji mengi."
Manispaa moja hivi karibuni ilikiri kuwa visima haramu vimekuwa tatizo.
Mwezi Mei mamlaka za mji wa Jakarta zilikagua majengo 80 kati kati mwa Jakarta, mtaa wa Jalan Thamrin kwenye majengo marefu, maduka na mahoteli. Iligundua kuwa majengo 56 yana visima vyao na 33 yalifanya hivyo bila vibali.
Picture of skyscrapers in Central JakartaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionIligundulika kuwa majengo 56 yana visima vyao na 33 yalifanya hivyo bila vibali.
Mamlaka pia zinamatumani kuwa Great Garuda, ukuta wa umbali wa kilomita 32 unaojengwa Jakarta utasaidia kuukoa mji huo kuzama kwa gharama ya dola bilioni 40.
Aerial picture of Jakarta's giant sea wallHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUkuta huu na kuzuia mafuriko mjini
Jan Jaap Brinkman mtaalamu anayefanya kazi na taasisi za maji huko uholanzi anasema suluhu ni kuzuia matumizi ya maji ya visima na kutegemea vyanzo vingine vya maji kama mvua na mito.
Picture of the unfinished construction of the sea wallHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUjenzi wa ukuta wa bahari unaendelea
Anasema Jakarta ni lazima ifanye hivyo ifikapo mwaka 2050 kuzuia mji kuzama zaidi.
Picture of the Citarum river filled with rubbishHaki miliki ya pichaAFP
Image captionVyanzoa vingine vya maji kama mito imechafuka sana
Sio ujumbe ambao unatiliwa maanani na Gavana wa mji wa Jakarta Anies Baswedan anasema njia nyingi inaweza kusaidia.
Anasema watu wanaweza kutumia maji ya visima kisheria kama wanaweza kurejesha maji hayo tena ardhini kwenye mfumo unaojulikana kama biopori.
Hapa ni wakati mtu anachimba shimo la upana wa sentimita 10 na lenye kina cha sentimita 100 kuruhusu maji kurudi tena ardhini.
Picture of a dike in North Jakarta.
Image captionUkuta unaozuia maji karibu na bahari
Kuna teknolojia ya kurejesha maji ya visima kwenye vyanzo vyake lakini ni ghali mno. Tokyo ulitumia mfumo huu wakati ardhi yake ilishuka sana miaka 50 iliyopita. Serikali pia ikadhibiti matumizi ya matumizi ya maji ya visima na biashara zikaaza kutumia maji ya mifereji. Kushuka kwa ardhi kukasitishwa.
Joko WidodoHaki miliki ya pichaBIRO PERS SETPRES
Image captionRais Joko Widodo anasema itachukua miaka mingi kusafisha mito ya Jakarta
Taarifa zaidi na Tom de Souza. michoro na Arvin Surpriyadi, Davies Surya, na Leben Asa.

About Author Mohamed Abu 'l-Gharaniq

when an unknown printer took a galley of type and scrambled it to make a type specimen book. It has survived not only five centuries.

No comments:

Post a Comment

Start typing and press Enter to search