Tetesi za soka Ulaya Ijumaa
Tetesi za soka Ulaya Ijumaa
Mshambuliaji wa Stoke na Uingereza
Peter Crouch, 36, analengwa kusajiliwa na Chelsea baada ya majeruhi
kumnyima Andy Carroll , 29, fursa ya kuhamia klabu hiyo.(Telegraph)
Chelsea
inataka kumsajili mshambuliaji wa Bosnia Edin Dzeko, 31, na beki wa
Itali Emerson Palmieri, 23, kutoka Roma. Wawili hao wanaweza kugharimu
jumla ya £77m. (Daily Star)Chelsea itamtumia mshambuliaji wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 24 kumsajili Edin Dzeko. (Sky Italia)
- Zinedine Zidane: Sioni Real Madrid bila Cristiano Ronaldo.
- Arsene Wenger adaiwa 'kuikosea heshima' Dortmund
- Neymar azomewa kwa kumnyima Cavani penalti
Alexis Sanchez amelazimika kufanya mazeozi na timu ya vijana huku mpango wa mchezaji huyo kuelekea Old Trafford ukiendelea kuchelewa. (Times)
United wanaiongoza Liverpool na Chelsea katika harakati za kumnunua kiungo wa kati wa Nice Jean-Michael Seri, 26, huku Manchester City pia ikimtaka mchezaji huyo wa Ivory Coast. (Mirror)
Brighton inamtaka mshambuliaji wa Uholanzi na PSV Jurgen Locadia, 24. (De Telegraaf - in Dutch)
Mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 24, atalazimilka kuwasilisha ombi la uhamisho ili kupata fursa ya kujiunga na Manchester United, kulingana na afisa mkuu wa Juventus Beppe Marotta. (La Gazetta Dello Sport - in Italian)
Winga wa Everton na mchezaji wa zamani wa Uingereza Aaron Lennon, 30, na mshambuliaji wa Leicester Islam Slimani, 29, wanalengwa na Newcastle ili kusajiliwa kwa mkopo. (Shields Gazette)
Besiktas pia ina hamu ya kumsajili Slimani na sasa Watford wamejiunga katika harakati za kumsajili mchezaji huyo wa Algeria (Daily Star)
West Brom wanafanya mazungumo ya kumsaini beki wa kulia wa Basle na Switzerland Michael Lang, 28. (Mail)
Mkufunzi wa Huddersfield David Wagner amepinga kufanyika kwa uhamisho wowote licha ya klabu hiyo kuhusishwa na uhamisho wa beki wa Borussia Dortmund na Serbia Neven Subotic, 29. (Huddersfield Examiner)
Arsenal inaelekea kuafikiana na mchezaji wa Ujerumani Mesut Ozil, 29, na kiungo wa kati Jack Wilshere, 26 kusaini kandarasi mpya. (Sun)
No comments:
Post a Comment