Mtu afariki baada ya 'kuigonga' ndege Tanzania
Mtu afariki baada ya 'kuigonga' ndege Tanzania
Mtu mmoja amefariki nchini Tanzania baada ya kuigonga ndege iliokuwa ikipaa katika uwanja wa ndege wa Mwanza
Akizungumza
kwa njia ya simu mmoja wa wafanyakazi wa kiwanja hicho cha ndege
ameielezea BBC kuwa mtu huyo alivuka mpaka na kuingia eneo la uwanja wa
ndege na moja kwa moja kwenye njia ya kurukia ndege ambapo alikutana
na ndege ya shirika la ndege la Fast Jest iliyokuwa inaruka kuelekea
jijini Dar es salaam.Jeshi la polisi jijini Mwanza linasema tukio hilo la aina yake lilitokea usiku majira ya saa tatu Januari 17 na baada ya kuruka rubani wa ndege iliyohusika aliwajulisha wenzake kwenye mnara wa kuongozea ndege uwanjani hapo juu ya tukio hilo
- Mwanamfalme wa Saudi Arabia afariki katika ajali ya ndege
- Ndege ndefu zaidi duniani yapata ajali
- Ndege iliowabeba waandishi wa habari yaanguka Kenya
Mpaka sasa haijafahamiki ilikuwaje mtu huyo akawepo kwenye njia ya kurukia ndege wakati ndege ilipokaribia kuruka licha ya ukaguzi wa njia hiyo kabla ya ndege hiyo kuruhusiwa kuanza safari yake.
Jeshi la Polisi nchini humo linaendelea na uchunguzi kubaini undani wa kisa hicho
Uwanja wa ndege wa Mwanza uko pembezoni mwa ziwa victoria na umepakana na makazi ya watu na kwa muda sasa umekuwa hauna uzio licha ya kuwa umekuwa ukitengenezwa kwa miaka kadhaa sasa
No comments:
Post a Comment