Tetesi za Soka Ulaya Jumatano
Tetesi za Soka Ulaya Jumatano
Lionel Messi amekataa ofa ya pauni
850,000 kwa wiki kutoka Manchester City kabla ya kusaini mkataba mpya na
Barcelona. (Marca - in Spanish)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp
anasema kuwa hana uhakika ikiwa mchezaji wa kiungo cha kati Philippe
Coutinho bado atakuwa Anfield baada ya mwezi Januari. Barcelona ilitoa
ofa mara tatu kwa raia huyo wa Brazil msimu huu. (Daily Star)Everton wamewaulizia Arsenal kuhusu mshambuliaji Theo Walcott, 28, ambaye badoa hajaanza kucheza msimu huu. (Daily Mail)
Chelsea wamepewa matumaini baada ya taarifa kuwa mlinzi wa Brazil Alex Sandro, 26, anataka kuhama Juventus. (Telegraph)
Ivan Perisic, 28, wa Manchester United amefichua kuwa Kocha wa Inter Milan Luciano Spalletti alijaribu kumshawishi asahame Italia badala ya kuhamia Old Trafford. (Mediaset via Manchester Evening News)
Southampton, Newcastle United na Crystal Palace wanammezea mate mlinzi wa Dandee Jack Hendry, 22. (Daily Mail)
No comments:
Post a Comment