Ndege ya Marekani ya B-1B bomber yawaonyesha ubabe Korea Kaskazini
Ndege ya Marekani ya B-1B bomber yawaonyesha ubabe Korea Kaskazini
Jeshi la Marekani limerusha ndege
yake aina ya B-1B bomber katika anga ya Korea Kusini kama sehemu ya
mazoezi ya pamoja ya angani katika hatua inayoonekana kama onyo kwa
Korea Kaskazini.
Mazoezi hayo ya kijeshi yanafanyika wiki moja
baada ya Korea Kaskazini kurusha kombora ililodai kuwa ni la masafa
marefu ambalo linaloweza kushambulia nchini Marekani.Marekani awali imerusha ndege hizo zenye uwezo wa juu kuonyesha ubabe baada ya majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini au majaribio ya mabomu ya nyuklia.
Pyongynag ambayo mara nyini hukashifu mazoezi ya pamoja ya Marekania na Korea Kusini, imeyataja mazoezi ya sasa kuwa uchokozi wa vita vya nyuklia.
Misukosuko imekuwa ikiongezeka tangu lifanyike jaribio la kombora mwezi uliopita lililosababisha lawama za kimataifa na onyo kutoka Marekani kuwa Korea Kaskazini itaharibiwa aabisa ikiwa vita vitatokea.
No comments:
Post a Comment