Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu
Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu
Real Madrid wanamwinda Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino kuweza kuchukua nafasi ya Zinedine Zidane. (Sun)
Arsenal
wanatarajiwa kuanza mazungumzo na waakilishi wa Jack Wilshere kuhusu
kuongezwa mkataba wa mchezaji huyo wa safu ya kati wa England kupita
msimu ujao. (Daily Mail)Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibatahimovic,36, ana karibu miaka 5 au 6 hivi ya kucheza kandanda kwa mujibu wa ajenti wake Mino Raiola. (FourFourTwo)
Liverpool wana mpango wa kutoa pauni milioni 4.5 kwa mchezaji wa safu ya kati Manor Solomon wa miaka 18 ambaye ameonyesha mchezo mzuri akiichezea Maccabi Petah Tikva. (Sun)
Aliyekuwa mlinzi wa Manchester United na England Gary Neville, anasema kuwa hawezi kamwe kurejea kwenye usimamizi wa kandanda (Manchester Evening News)
Mshambuliaji wa Newcastle raia wa Uhispania Mikel Merino,21. yuko sawa kabisa kuweza kuwavutia Real Madrid na Barcelona (Independent)
Meneja wa Real madrid Zinedine Zidane amemuambia rais wa klabu hiyo Florentino Perez kuwa hataki mchezaji yeyote kuuzwa wakati wa msimu wa mwezi Januari. (Don Balon - in Spanish)
Manchester United hawako wazuri kama Manchester City au Tottenham, kulingana na wing'a wa Huddersfield Tom Ince, 25. (Daily Star)
No comments:
Post a Comment