Uamuzi kuhusu kesi ya uchaguzi wa urais Kenya
Uamuzi kuhusu kesi ya uchaguzi wa urais Kenya
Ulinzi umeimarisha ndani na nje ya majengo ya Mahakama ya Juu jijini Nairobi ambapo majaji wanatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyotangazwa na IEBC.
Mpiga picha wetu Rod Mcleod ametutumia picha hizi za maafisa wakishika doria nje ya majengo hayo.
BBC
BBC
Wakati wa kusikizwa kwa kesi, kulikuwa na mvutano kuhusu kukaguliwa kwa mitambo ya tume ya uchaguzi.
Upinzani ulikuwa umedai mitambo hiyo ilidukuliwa na kuingiliwa ili kumfaa Bw Kenyatta.
Tume hiyo baadaye jioni siku ya Jumanne iliwapa wataalamu wa upinzani Nasa fursa ya kukagua mitambo hiyo ingawa bado kulikuwa na kutoelewana kuhusu kiwango ambacho mitambo hiyo ilifunguliwa.
Sikiliza zaidi: Mvutano kuhusu kufunguliwa kwa mitambo ya tume Kenya
AFP/Getty
Mahakama ya Juu Kenya ina majaji saba ambao walianza kusikiliza kesi hiyo ya matokeo ya uchaguzi wa urais.
Majaji hao ni:
- Jaji Mkuu David Maraga
- Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu
- Jaji Prof Jackton Boma Ojwang
- Jaji Mohammed K. Ibrahim
- Jaji Njoki S. Ndungu
- Jaji Dkt Smokin C. Wanjala
- Jaji Isaac Lenaola
Jaji Mohammed Ibrahim aliugua siku ya mwisho ya kusikizwa kwa kesi hiyo Jumanne wiki hii.
Kulikuwa na wagombea wanane katika uchaguzi wa urais uliofanyika tarehe 8 Agosti.
Matokeo ya uchaguzi huo yalitangazwa Ijumaa tarehe 12 Septemba na mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati.
Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:
- Ekuru Aukot 27,311 (0.18%)
- Abduba Dida 38,093 (0.25%)
- Cyrus Jirongo 11,705 (0.08%)
- Japheth Kaluyu 16,482 (0.11%)
- Uhuru Kenyatta 8,203,290 (54.27%)
- Michael Wainaina 13,257 (0.09%)
- Joseph Nyagah 42,259 (0.28%)
- Raila Odinga 6,762,224 (44.74%)
Waliokuwa wamejiandikisha kushiriki katika uchaguzi huo ni 19,611,423 lakini waliopiga kura walikuwa 15,073,662 ambao ni sawa na asilimia 78.91.
Idara ya Mahakama imesema majaji wa Mahakama ya Juu wataanza kutoa uamuzi kuhusu kesi hiyo iliyowasilishwa na upinzani saa tano leo.
Leo ndiyo siku ya mwisho kikatiba kwa mahakama hiyo kutoa uamuzi.
No comments:
Post a Comment