[TRENDING][10]

CENTER OF ICT
ENTERTAINMENT
GOSSIP
NEWZ
SPORTS
VIDEOS

Zidane afikia rekodi Del Bosque ya kutwaa mataji saba Real Madrid

Zidane afikia rekodi Del Bosque ya kutwaa mataji saba Real Madrid


Madrid, Hispania. Baada ya kuiongoza Real Madrid kutwaa ubingwa wa Hispania Super cup kwa kuifunga Barcelona kwa jumla ya mabao 5-1, Zinedine Zidane ameweka rekodi ya kunyakuwa mataji saba sawa na Vicente Del Bosque.
Real chini ya Zidane imefanikiwa kutwaa mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa, mawili ya UEFA Super Cups, huku akichukua mara moja moja Kombe la Dunia la Klabu, La Liga na Hispania SuperCup.
Mataji hayo yanafanya Zidane kuifikia rekodi ya kocha Vicente Del Bosque na sasa anaisaka rekodi ya Luis Molowny aliyetwaa mataji nane na Miguel Munoz aliyeiongoza Real kutwaa makombe 14.
Zidane anaiweka rekodi hiyo ikiwa ni chini ya miaka miwili tangu alipochukua jukumu hilo, hivyo kuna uwezekano akachukua mataji mengi zaidi na kuwa kocha mwenye mafanikio zaidi katika kikosi cha Real.
Nafasi yake nyingine ya kutwaa kombe inakuja Desemba wakati Real itakaposhiriki Kombe la Dunia la Klabu, endapo Zidane atashinda taji hilo itakuwa ni mara yake ya pili kuchukua na kuwanya kuwa kocha bora zaidi.

About Author Mohamed Abu 'l-Gharaniq

when an unknown printer took a galley of type and scrambled it to make a type specimen book. It has survived not only five centuries.

No comments:

Post a Comment

Start typing and press Enter to search