[TRENDING][10]

CENTER OF ICT
ENTERTAINMENT
GOSSIP
NEWZ
SPORTS
VIDEOS

We bisha tu, Mayweather anakuja Bongo aisee

We bisha tu, Mayweather anakuja Bongo aisee

ULE mpango wa nguli wa ndondi duniani, Floyd Mayweather, kutua hapa nchini umeanza kukamilika na inaelezwa atafanya ziara jijini Dar es Salaam akitokea Ghana, atakakoenda mara baada ya pambano lake na Conor McGregor la Agosti 26.
Baada ya pambano hilo litakalofanyika Las Vegas, Marekani, Mayweather ‘Money Man’ atazuru Ghana alikokuwa aende tangu Juni lakini akaisogeza mbele safari hiyo ili kupisha maandalizi yake ya kupigana na McGregor.
Mratibu wa ujio wa bondia huyo nchini, Juma Ndambile ‘Chief’ amesema kuwa mipango ya kumpokea mbabe huyo inaendelea vizuri kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.
“Tumekwishazungumza na kampuni ya Upscale Entertainment ambayo ndiyo inasimamia safari za Mayweather,” alisema Ndambile, promota maarufu wa ngumi nchini.
“Nilikuwa Ghana, tumekubaliana na kuwa akitoka huko aje Tanzania. Kuna mambo tuliyokubaliana nao kuhusu safari hiyo na yanakwenda vizuri. Kikubwa tunasubiri menejimenti ya bondia huyo kutangaza tarehe rasmi ya kufika Ghana ili masuala mengine yafuatie.”
Aliongeza kuwa ziara hiyo ni sehemu ya mikakati yake aliyoipanga baada ya kuhudhuria mkutano mkuu wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) uliofanyika Desemba mwaka jana kule Marekani.
“Tunaanza na Mayweather, lakini kuna mengi yatakuja baadaye kwani kule nilizungumza pia na akina Lenox Lewis, Amir Khan, Wladimir Klitschko, Evander Holyfield na mapromota maarufu kama Don King na Jay Mathews. Wote hao wana nia ya kuja nchini kwa ajili ya kuona vivutio vya utalii na kuwekeza,” aliongeza.     

About Author Mohamed Abu 'l-Gharaniq

when an unknown printer took a galley of type and scrambled it to make a type specimen book. It has survived not only five centuries.

No comments:

Post a Comment

Start typing and press Enter to search