[TRENDING][10]

CENTER OF ICT
ENTERTAINMENT
GOSSIP
NEWZ
SPORTS
VIDEOS

TANGA: Rais Magufuli azindua stendi mpya ya mabasi Korogwe. Prof. 'Maji Marefu' atamani atawale miaka 20

TANGA: Rais Magufuli azindua stendi mpya ya mabasi Korogwe. Prof. 'Maji Marefu' atamani atawale miaka 20

 IMG_2388.JPG

Rais Magufuli anaendelea na ziara yake mkoani Tanga leo ikiwa siku ya tano. Leo yuko wilayani Korogwe kufungua stendi mpya ya mabasi.
======

Miongoni mwa walioongea mpaka sasa ni mbunge wa Korogwe, Stephen Ngonyani maarufu kama Maji Marefu ambae ametoa hoja ya Rais Magufuli kuongoza nchi kwa miaka ishirini kwani kumi ya sasa haitamtosha na anaeongea kwa sasa ni mbunge wa Bumbuli ambae yeye katilia mkazo hoja ya utaifa na kutoa historia fupi jinsi walivyoinyonya Afrika na kisha kuwa washirika wa maendeleo ndani ya muda mfupi.

Anaeongea kwa sasa ni waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na anasema Korogwe na maeneo ya milimani ni moja ya sehemu zinazobeba kura nyingi za CCM mkoa wa Tanga tofauti na eneo la Pwani. Amedai hata yeye kura zake za viti maalum zimetoka huko ila watu wa ukanda wa Pwani ni waswahili kidogo.
Anaeongea kwa sasa ni Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na anaelezea sifa ya stendi hiyo na anawapa hongera na kuonyesha matumaini yake kuwa wataitunza vizuri kwani watu wa Korogwe hawana tabia ya uharifu.

Rais Magufuli: Pasiwepo na vikwazo vya watu kupata maduka hayo au masharti magumu, wasije wakapata watu wasiotoka hapa Korogwe, kama Mkurugenzi una mtu wako anatoka mahala pengine anataka duka, mmalizie huko huko.

Kandarasi atakaezembea hatutasita kuwatumbua, tunataka fedha za watanzania zifunguke kama zilivyopangwa. Kazi hii imefanywa na kandarasi wazalendo, nawapongeza sana.

Mambo yakienda vizuri, wapiga debe debe watazungumza.

About Author Mohamed Abu 'l-Gharaniq

when an unknown printer took a galley of type and scrambled it to make a type specimen book. It has survived not only five centuries.

No comments:

Post a Comment

Start typing and press Enter to search