Kwa Picha: Picha bora Afrika wiki hii 18 - 24 Agosti 2017
Kwa Picha: Picha bora Afrika wiki hii 18 - 24 Agosti 2017

Katika mji mkuu wa Ghana, Accra, mwanamke huyu alikuwa amevalia mahsusi kuhudhuria Tamasha ya Sanaa ya Barabarani ya Chale Wote.

Mamia ya wasanii wenyeji na kutoka nje ya nchi walihudhuria tamasha hiyo siku ya Jumamosi ambapo waliwatumbuiza waliohudhuria kwa sarakasi, vichekesho, kucheza ngoma na mengine mengi.

Siku iyo hiyo, wanawake hawa walikuwa wana furaha tele katika Tamasha ya Jollof katika mji mkuu wa Nigeria, Lagos. Ilikuwa fursa kwa wapenzi wa Jollof, chakula kinachotayarishwa kwa kutumia mchele, ambacho ni maarufu sana Afrika Magharibi kuonja ladha mbalimbali za chakula hicho.

Na siku iyo hiyo, katika mji mkuu wa Angola, Luanda, wafuasi wa chama tawala cha MPLA wanaonekana wakiwa na furaha katika mkutano wa kampeni. Mgombea wa chama hicho Joao Lourenco anatarajiwa kuwa rais baada ya Jose Eduardo dos Santos kutangaza atastaafu baada ya kuongoza wka miaka 38.

Na siku iliyofuata, wafuasi wa kiongozi mkuu wa upinzani Isaias Samakuva, wanaonekana wakuwa na jogoo mweusi, nembo ya chama cha Unita chake Samakuva.

Hayo yakijiri, nchini kenya wafuasi wa kiongozi mkuu wa upinzani Raila Odinga waliandamana Nairobi siku ya Ijumaa. Upinzani umewatuhumu polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi kukabiliana na waandamanaji walioandamana kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa tarehe 8 Agosti. Polisi wamekanusha tuhuma hizo.

Jumamosi, rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, 74, alilakiwa na baadhi ya magavana wa majimbo ya nchi hiyo katika uwanja mkuu wa Abuja baada yake kurejea kutoka Uingereza alikokuwa anapokea matibabu kwa miezi mitatu.

Nchini Burkina Faso, katika mji mkuu wa Ouagadougou, mwandamanaji anabeba bango lenye ujumbe 'Hatutaki unyama' wakati wa maandamano Jumamosi kulalamika kuuawa kwa watu 18 katika shambulio la kijihadi katika mgahawa mmoja maarufu wa Kituruki.

Na katika picha hii iliyotolewa Ijumaa, watoto wanaonekana wakicheza katika Mto Chari katika mji mkuu wa Chad, N'Djamena.

Siku hiyo pia, wazazi hawa nchini Misri walikuwa wanawafunza watoto wao kuogelewa mjini Cairo.
Picha kwa hisani ya AFP, EPA, Getty Images na Reuters
No comments:
Post a Comment