Jumba refu lachomeka Dubai
Jumba refu lachomeka Dubai
Moto mkubwa umelichoma mojawapo ya jumba refu duniani Torch Tower huko Dubai UAE kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka miwili.
Picha zilizowekwa katika mitandao ya kijamii zilionyesha moto huo ukisambaa hadi katika jumba hilo huku vifusi vilivyokuwa vikichomeka vikianguka.
Mamlaka baadaye ilisema kuwa wafanyikazi walifanikiwa kuwaondoa watu na wakafanikiwa kuudhibiti moto huo.
- Kenya kujenga jumba refu zaidi barani Afrika
- Marekani yaadhimisha shambulio la Septemba 11
- Jumba la Nyerere makao makuu ya AU
Haijulikani ni nini kilichosababisha moto huo katika mojawapo ya jumba refu dunaini.
Hakuna majeraha yoyote yalioripotiwa kufikia sasa katika jumba hilo la Torch Tower ,kulingana na mamlaka ya Dubai iliotuma ujumbe katika Twitter.
Jumba hilo la Torch Tower liliharibiwa na moto mwengine 2015.
No comments:
Post a Comment