Wanawake 'wacheza utupu' watumbuiza wafungwa Afrika Kusini
Wanawake 'wacheza utupu' watumbuiza wafungwa Afrika KusiniWafungwa katika gereza la Sun City nchini Afrika Kusini, walitumbuizwa na 'wacheza utupu' kama sehemu ya hafla rasmi.
Picha zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zinaonyesha wanawake wawili waliovalia nusu uchi wakiwaburudisha wafungwa katika jela hiyo mjini Johannesburg.
Idara ya huduma ya kurekebisha watu tabia imethibitisha kwamba kisa hicho kinachoonyesha picha za mahabusi wakiwa wamekumbatiana na akina dada ni kisa cha ukweli kilichotokea katika jela.
Uchunguzi kamili umeanzishwa, afisa wa idara ya magereza James Smalberger ameambia wanahabri.
"Hatuwezi kuvumilia yale ambayo tumeyaona katika mitandao ya kijamii tangu Jumamosi," Bw Smalberger, ambaye ni kaimu kamishna wa idara ya taifa ya magereza amesema.
Askari jela 13 wamesimamishwa kazi na watachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni na sheria za idara hiyo.
Hafla hiyo iliyoandaliwa 21 Juni ilikuwa sehemu ya maadhimisho ya Mwezi wa Vijana, ambayo ni sehemu ya mpango unaokusudiwa kuwarekebisha tabia wafungwa.
Lakini wanawake hao - na mavazi yao - waliwashangaza maafisa.
Msemaji wa idara ya magereza ya Gauteng Ofentse Morwane aliambia TimesLive: "Wanenguaji viuno walifika, tuliona walikuwa wanavalia nguo za ndani. Waliandaa igizo kama la kuvua nguo hivi na wahalifu hao."
Picha za wanawake hao wakiwaburudisha wafungwa zilianza kusambaa mitandao ya kijamii wikendi, na kusababisha uvumi kwamba huenda labda maisha ni mazuri gerezani kuliko nje ya jela.
No comments:
Post a Comment