Trump: Wanaobadili jinsia hawawezi kuhudumu katika jeshi
Trump: Wanaobadili jinsia hawawezi kuhudumu katika jeshi.
Rais Trump ametangaza kuwa Jeshi la Marekani halitawaruhusu watu wanaobadilisha jinsia zao kuendelea kufanya kazi ya aina yoyote jeshini.
Katika taarifa kadhaa kwenye mtandao wa Twitter, Bwana Trump alisema kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kufanya mashauriano na maafisa wa vyeo vya juu jeshini.
Alisema watu wanaobadilisha jinsia zao wataligharimu jeshi kimatibabu na kuvuruga maisha ya kawaida jeshini.
Mapema mwezi huu waziri wa Ulinzi wa Marekani, James Mattis, alisimamisha uajiri wa watu wanaobadilisha jinsia zao kwa miezi sita.
- Waliobadili jinsia kuajiriwa na jeshi mwaka ujao Marekani
- Marekani yaiangusha ndege ya jeshi la Syria
- Jeshi la Marekani lasaidia jeshi la Ufilipino kupigana na wanamgambo
- Mchungaji mpinga mapenzi ya jinsia moja akimbia mafuriko
Shirika moja kwa jina Independent Rand Corporation linakadiria kwamba mnamo mwaka 2016 wanajeshi 2,450 kati ya wanajeshi milioni 1.2 ni watu waliobadili jinsia ijapokuwa wanaharakati wanasema kuwa idadi hiyo huenda ikawa juu.
Katika msururu wa ujumbe wa Twitter bwana Trump alisema: Baada ya majadiliano na majenerali pamoja na wataalam wa kijeshi tafadhali nawashauri kwamba Marekani haitaruhusu ama kukubali watu wanaobadili jinsia kuhudumu katika kiwango chochote cha jeshi nchini Marekani.
Jeshi linafaa kuwa na lengo moja la kuibuka mshindi na haliwezi kugubikwa na mzigo wa gharama ya juu ya matibabu ambayo watu wanaotaka kubadili jinsia wangehusishwa nayo.
Marufuku hiyo kwa wapenzi wa jinsia moja wanaojulikana kama ''don't Ask don't tell'' iliondolewa 2011.
Aaron Belkin ambaye ni mkurugenzi wa kituo cha Palm center kinachoongoza kuhusu maswala ya jinsia katika jeshi aliambia BBC kwamba hatua hiyo ya Trump itawalazimu wanajeshi waliobadili jinsia kuishi kama wapenzi wa jinsia moja chini ya ''Dont ask dont tell''.
''Dont ask Dont tell ilikuwa sera mbaya ilioathiri jeshi kwa kipindi cha miongo miwili'' ,alisema bwana Belkin.
Haijulikani ni kwa nini Rais anataka kurudisha tena sera hiyo kwa wanajeshi waliobadili jinsia, wakati ambapo ushahidi wote unaonyesha kuwa sera hiyo kwa ujumla itawafaidi wanajeshi huku ubaguzi ukiliathiri jeshi hilo.
Baadhi ya wanachama wa Republican walipinga watu wanaobadili jinsia kujiunga na jeshi.
No comments:
Post a Comment