Trump ajutia kumteua mwanasheria mkuu Jeff Sessions
Trump ajutia kumteua mwanasheria mkuu Jeff SessionsRais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa hangemteua Jeff Sessions kama mwanasheria mkuu, kama angejua kuwa angejiondoa kutoka kuongoza uchunguzi kuhusu Urusi.
Bwana Trump ameiambia New York Times kuwa hatua ya Bwana Sessions haijakuwa nzuri kwa urais.
Bwana Sessions alijiondoa baada ya kukiri kuwa alikutana na balozi wa Urusi.
Alisema leo Alhamisi kuwa hawezi kujiuzulu na ataendelea kuongoza idara ya sheria vyema.
Bwana Sessions alikuwa mmoja wa wale walimuunga mkono zaidi Bwana Trump.
- Maseneta wamuidhinisha mwanasheria mkuu wa Trump
- Sessions: Sikufanya mikutano ya siri na maafisa wa Urusi
- Mwanasheria mkuu US atakiwa kujiuzulu kwa kuwasiliana na Urusi
- Democrats wamtaka mwanasheria mkuu kujiuzulu Marekani
Licha ya gavana huyo wa zamani wa Alabama kuwa na jukumu la kutekeleza ajenda ya Rais kama mwanasheria mkuu, Bwana Trump mwenyewe anamlaumu wa kuruhusu kuwepo kwa uchunguzi huru ambao umehujumu Urais.
Aliyekuwa mkurugenzi wa FBI James Comey ambaye mwenyewe alilengwa na Trump alifichua kuwa kundi la kampeni ya Trump lilikuwa chini ya uchunguzi.
No comments:
Post a Comment