Taarifa za kuzushiwa kifo zimemfikia King Majuto, katuma Ujumbe ‘Sote tutakufa
Taarifa za kuzushiwa kifo zimemfikia King Majuto, katuma Ujumbe ‘Sote tutakufa.
Siku chache zilizopita kulikuwa na taarifa za uzushi zilizokuwa zinaenea kumuhusu Mchekeshaji maarufu Bongo, Amri Athuman ‘King Majuto’ zikidai kuwa amefariki kutokana na kuumwa kwa muda.
Baada ya kusambaa kwa taarifa hizo zilimfikia mwigizaji na mchekeshaji Mboto Hajiambaye alisafiri hadi Tanga kujua kinachoendelea na kupost picha kwenye Instagram yake akiwa na Mzee Majuto nyumbani kwake na kutueleza hakuwa amekufa kama ilivyozushwa ingawa alikuwa mgonjwa lakini aliyekuwa na ahueni.
Sasa Ayo TV na millardayo.com zilifanya jitihada kumpata King Majuto ili kufahamu hali yake na kuhusu taarifa za kuzushiwa kifo kama zilimfikia na alivyozipokea:>>>”Mimi ni mzima niko nyumbani kwangu, nimeshatoka Hospitali. Nilipelekwa kwa maradhi ya henia, nimeshafanyiwa upasuaji na nyuzi zimeshatoka zote. Niko nyumbani nafanya mazoezi na kula kurudisha nguvu za mwili.
“Kitu ambacho kimeniudhi ni kwamba kuna Watanzania simu hawana kazi nazo. Wanapokuwa hawana kazi nazo wanaposti post vitu vya kipumbavu waache sio vizuri.”
No comments:
Post a Comment