Simba apatikana akimnyonyesha mwana wa Chui Tanzania
Simba apatikana akimnyonyesha mwana wa Chui Tanzania
Mwana wa chui hawezi kubadili madoa doa katika ngozi yake lakini simba huyo hajali hilo.
Picha hizi ni za kwanza kuchukuliwa simba akimnyonyesha mwana wa chui kutoka jamii nyengine ya wanayama, kisa kisicho cha kawaida.
Wawili hao walionekana na Joop Van Der Linde mgeni katika katika eneo la Ndutu safari Lodge nchini Tanzania katika eneo la uhifadhi la wanyma pori la Ngorongoro.

Simba huyo amewekewa mfumo wa GPS katika shingo yake ili kutambua anakokwenda na ana watoto watatu waliozaliwa kati ya mwezi Juni 27-28.


Sina kisa chengine chochote nikijuacho kati ya familia ya mnyama paka kwa mfano pale ambapo mnyama mmoja amechukua mwana wa mnyama mwengine katika familia hiyo hiyo na kumnyonyesha.
Simba wengi wa kike huwauwa watoto wa chui wanapokutana nao, na huwaona kama wapinzani katika mapambano ya kutafuta chakula.
Daktari Hunter anasema Nosikitok ana watoto wachanga walio na umri sawa na mwana huyo wa chui wakiwa na wiki mbili hadi tatu hivi.

Alimchukua mwana huyo na kumlea kama wake na humlindi dhidi ya shambulio lolote
No comments:
Post a Comment