Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu amekamatwa.
Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu amekamatwa.
Hakuna sababu zilizotolewa kwa kukamatwa kwa Lisu ,licha ya kwamba hatua hiyo inajiri siku tatu baada ya kumwita rais Magufuli ''dikteta''.
Siku ya Jumatatu bwana Lissu aliwaambia wanahabari kwamba kukamatwa mara kwa mara kwa viongozi wakuu wa upinzani kunalenga kukandamiza upinzani wowote kwa rais Magufuli.
Ametaka wananchi kumtenga ''dikteta'' huyo na serikali yake kisiasa, kidiplomasia na kiuchumi kulingana na chombo cha habari cha AFP.
Msemaji wa serikali Hassan Abbas alijibu matamshi ya Lissu mapema wiki hii akisema katika taarifa kwamba serikali haitakubali mtu ama kundi la watu kutumia vibaya uhuru wa kujieleza.
Bwana Lissu ambaye ni mwanachama wa chama kikuu cha upinzani Chadema, anahudumu kama kiranja mkuu wa upinzani bungeni na pia anaongoza muungano wa mawakili.
Alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam akijaribu kupanda ndege kuelekea Rwanda, msemaji wa Chadema ameambia AFP.
No comments:
Post a Comment