Kingine kutoka kwa Mtanzania aliyesoma kwa ada ya Milioni 365
EXCLUSIVE: Kingine kutoka kwa Mtanzania aliyesoma kwa ada ya Milioni 365
Kama ndio
kwanza unakutana na hii, nakukumbusha kwamba Benjamin Fernandes ni
Mtanzania ambaye anaingia kwenye historia kubwa kwenye upande wa elimu
baada ya kupata ufadhili wa kusoma chuo kikuu cha biashara Stanford
Graduate School of Business nchini Marekani.
Ni
Mtanzania wa kwanza kupata udhamini wa masomo (Scholarship) ya heshima
kusoma chuo hicho kwa ada ya dola 160,000 za Marekani ambazo ni zaidi ya
milioni 365 za Tanzania. Scholarship kama hiyo imetolewa kwa watu nane
tu kutoka Afrika akiwemo yeye.