GUMZO la moto Kagera nalo noma…huunguza nyumba na migomba mchana
GUMZO la moto Kagera nalo noma…huunguza nyumba na migomba mchana
Story kubwa kutoka Mkoa wa Kagera ni baada ya Wilaya ya Muleba kuingia kwenye headline kufuatia tukio la kushangaza ambapo moto ambao haujafahamika chanzo chake umeteketeza nyumba za watu mchana huku ikiwa si mara ya kwanza kwa tukio kama hilo.
Diwani wa Kata ya Mayondwe Method Bakuza amesema kuwa matukio ya nyumba kuteketea kwa moto wa ghafla yalianza May 4 mwaka huu katika kitongoji cha Ibila katika kijiji cha Bugasha ambapo hadi leo nyumba 12 zimeteketea bila kujulikana chanzo cha moto huo.
Tukio lingine la kushangaza ni kuwa moto huo hutokea mchana na unateketeza nyumba pamoja na migomba inayokuwa jirani na zaidi ya kuteketeza mali hakuna madhara mengine kwa binadamu na huwa mkali ambao huwa vigumu kuuzima.
ponyeza hapa kutazama.
https://youtu.be/T2XMmtTC6aY