[TRENDING][10]

CENTER OF ICT
ENTERTAINMENT
GOSSIP
NEWZ
SPORTS
VIDEOS

meli ya japan yasindikiza meli za marekani


Japan imetuma meli ya kubwa zaidi ya kivita baharini, hatua yake ya kwanza ya aina hiyo tangu kupitishwa kwa sheria mpya yenye utata iliyowezesha taifa hilo kuanza kupanua uwezo wa jeshi lake.
Meli hiyo kubwa ya kubeba helikopta ambayo imepewa jina Izumo imetumwa kuifuata meli ya kubeba mizigo na vifaa vya kijeshi ya Marekani ambayo inapitia katika maeneo ya bahari ya Japan.
Meli hiyo ya Marekani inaelekea kufikisha mafuta kwa meli nyingine za taifa hilo zinalohudumu eneo hilo, ikiwemo meli yake kubwa ya kubeba ndege ya Carl Vinson na meli zinazoandamana na meli hiyo karibu na rasi ya Korea.
Korea Kaskazini imetishia kuizamisha Carl Vinson pamoja na nyambizi ya Marekani, huku wasiwasi ukiendelea kuongezeka eneo hilo.
Aidha, taifa hilo lilifanya jaribio la kurusha kombora ambalo lilifeli Jumapili, licha ya kuonywa mara kadha na Marekani na nchi jingine dhidi ya kufanya majaribio ya makombora au majaribio ya silaha za nyuklia.
Mwandishi wa BBC Rupert Wingfield-Hayes aliyepo mjini Tokyo anasema Izumo ndiyo ambayo ni fahari ya jeshi la wanamaji la Japan, na kufikia sasa ndiyo meli kubwa zaidi ya jeshi hilo.
Izumo ina urefu wa mita 249 na inaweza kubeba helikopta hadi tisa.
Inafanana sana na meli za kivita za kushambulia adui majini za Marekani ambazo zinamilikiwa na Marekani, gazeti la Japan Times linasema.
Shirika la habari la Kyodo limesema meli hiyo imeondoka kwenye kambi yake eneo la Yokosuka kusini mwa Tokyo kwenda kuungana na meli hiyo ya kusafirisha bidhaa za jeshi la Marekani, na kwamba itaisindikiza hadi kwenye pwani ya Shikoku magharibi mwa Japan.
Chini ya Waziri Mkuu Shinzo Abe, Japan inaanza kujiimarisha kijeshi kufikia kiwango ambacho inaruhusiwa kimataifa, na huku wasiwasi ukiongezeka katika rasi ya Korea, bw Abe anaonekana kuwa makini sana kujaribu kutumia sheria mpya zinazoikubalia serikali kuimarisha jeshi la nchi hiyo kwa mara ya kwanza, mwandishi wetu anasema

About Author Mohamed Abu 'l-Gharaniq

when an unknown printer took a galley of type and scrambled it to make a type specimen book. It has survived not only five centuries.

No comments:

Post a Comment

Start typing and press Enter to search