PSG Yatenga Paundi Milioni 90 Kumnyakua N’Golo Kante Kutoka Chelsea
PSG Yatenga Paundi Milioni 90 Kumnyakua N’Golo Kante Kutoka Chelsea

MATAJIRI wa jiji la Paris, Paris Saint-Germain wanajipanga kumnyakua kiungo mkabaji wa klabu ya Chelsea, N’Golo Kante kwa dau la paundi milioni 90 mwishoni mwa msimu huu.
PSG wanamtaka Kante baada ya Thiago Motta mwenye umri wa miaka 35 kuwa mbioni kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huku Marco Verratti akiwa kwenye orodha ya wachezaji wanaotakiwa na Barcelona kwa udi na uvumba.
Kante amejiunga na Chelsea akitokea Leicester City mwaka 2016 ambapo alishinda taji la Ligi Kuu ya Uingereza chini ya kocha Claudio Ranieri kabla ya kushinda taji lingine msimu uliopita chini ya kocha Antonio Conte akiwa na kikosi cha Chelsea.
Mfaransa huyo aliyeshinda tuzo za Mchezaji bora wa EPL msimu uliopita ana mkataba na mabingwa hao wa Uingereza unaomalizika mwaka 2021.
No comments:
Post a Comment