Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu
Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu
Manchester City wanaamini kuwa wanaweza kumpata mchezaji wa kiungo cha kati wa Real Madrid, Isco, 25, licha ya yeye kusaini mkataba wa muda mrefu huko Bernabeu. (Don Balon, via Daily Express)
Huku Meneja wa Burnley Sean Dyche akihusishwa na kuchukua kazi huko Everton, mlinzi Stephen Ward amesema kumpoteza itakuwa pigo kubwa. (Times - subscription required)
Huenda meneja wa Sunderland Simon Grayson akafutwa ikiwa klabu yake haitaishinda Bolton siku ya Jumanne. (Daily Star)
Meneja wa Manchester United anasema kuwa hana uhakika ikiwa Paul Pogba atakuwa sawa kucheza. (Daily Mirror)
Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale huenda akakosa mechi dhidi ya klabu yake ya zamani Tottenham katika Champions League siku ya Jumatano. (Times - subscription required)
No comments:
Post a Comment