Mbunge wa CCM Lazaro Nyalandu ajiuzulu Tanzania
Mbunge wa CCM Lazaro Nyalandu ajiuzulu Tanzania
Mbunge wa chama tawala nchini
Tanzania CCM Lazaro Nyalandu amejiuzulu wadhifa wake, na kusema kwamba
anataka kuhamia chama cha upinzani Chadema.
Bw Nyalandu, Aliyekuwa
Waziri wa Mali Asili na Utalii wakati wa serikali ya awamu ya Tano
nchini Tanzania amesema kupitia taarifa kwamba amejuzulu nyadhifa zake
zote ndani ya chama cha mapinduzi CCM ikiwemo ubunge.Nyalandu ambaye kabla ya maamuzi hayo ya kujiuzulu alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini amesema amechukua uamuzi huo kutokana na kutokuridhishwa na mwendo wa siasa nchini Tanzania, ukiukwaji wa haki za kibinaadamu, ongezeko la vitendo vya kidhalimu dhidi ya raia na kutokuwepo kwa mipaka baina ya mihimili ya dola - Serikali, Bunge na Mahakama.
Katika taarifa yake ya kujiuzulu aliyoiweka katika ukurasa wake wa Facebook, Nyalandu amesisitiza umuhimu wa nchi hiyo kupata katiba mpya.
"Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna namna yeyote ya kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali," amesema.
- Nnauye: Nilijua kuwa kuna gharama
- Magufuli amfuta kazi waziri wa nishati
- Ripoti ya Madini:Rais Magufuli amshauri Waziri ajiuzulu
"Ni imani yangu, kamwe hayatakuwa ya bure maneno haya, wala uamuzi huu niufanyao mbele ya Watanzania leo."
Nyalandu anaingia katika orodha ya mkururu wa viongozi wa juu wa CCM waliokihama chama hicho na kuhamia chama kikuu cha upinzani nchini humo Chadema tangu mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment