[TRENDING][10]

CENTER OF ICT
ENTERTAINMENT
GOSSIP
NEWZ
SPORTS
VIDEOS

Benki ya Dunia: Tanzania ina nafasi gani katika kukua kwa Bara la Africa?

Benki ya Dunia: Tanzania ina nafasi gani katika kukua kwa Bara la Africa?


Benki ya Dunia imeandaa semina kuzungumzia 'Kukua kwa bara la Africa: Kuwekeza katika Ujuzi na miundombinu ya Uwekezaji' (Africa's Growth: Centering Skills and Infrastructure Investment).

Mjadala huu utafanyika hapo kesho (November 7) saa nane mchana hadi saa kumi jioni, Ukumbi wa Nkurumah, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Semina hii ya Benki Kuu imewaandaa watoa mada;
  • Prof. Rwekaza Mukandala kama muendesha Mjadala
  • Dkt. Albert G. Zeufack kama Muwasilisha Mada
  • Prof. Michael Ndanshau na Prof Samuel Wangwe kama wachochea mjadala/mada.
Mjadala huu, ni nafasi nzuri kuweza kutafakari na kutambua nchi yetu pendwa ya Tanzania ina nafasi ipi katika kukua kwa Africa haswa katika kuwekeza kwenye Ujuzi na Miundombinu ya Uwekezaji.

JamiiForums tutawarushia mjadala huu moja kwa moja kupitia 'Live stream' hapa na pia tutawawasilishia mada itakayo report kinachojiri live.

Mjadala huu ni wazi kwa wote watakaopenda kushiriki, aidha kwa kufuatilia hapa JamiiForums ama kwa kuhudhuria hapo Chuo Kikuu (UDSM).

About Author Mohamed Abu 'l-Gharaniq

when an unknown printer took a galley of type and scrambled it to make a type specimen book. It has survived not only five centuries.

No comments:

Post a Comment

Start typing and press Enter to search