[TRENDING][10]

CENTER OF ICT
ENTERTAINMENT
GOSSIP
NEWZ
SPORTS
VIDEOS

Taarifa ya Uchunguzi wa Almasi uliokamatwa Uwanja wa ndege Dar, Almasi yenye thamani ya dola mil 29 yataifishwa

Taarifa ya Uchunguzi wa Almasi uliokamatwa Uwanja wa ndege Dar, Almasi yenye thamani ya dola mil 29 yataifishwa


DJRWG-IXcAAeSnB.jpg

Kutoka uwanja wa ndege, Dar almasi iliyokamatwa ikiwa inataka kusafirishwa kwenda nje ya nchi. Ilisemwa ina thamani ya dola za kimarekani milioni 14 lakini kamati imebaini ina thamani ya dola milioni 29. DAR: Almasi yenye thamani ya Sh. Bilioni 32 yanaswa airport ikisafirishwa kwenda Ubelgiji

(Jeshi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema kuwa linashikilia watu wanne kwa kushukiwa kutaka kusafirisha madini aina ya almasi yenye thamani ya shilingi bilioni 32.8 bila kufanyiwa ukokotoaji sahihi.

Zoezi hilo limefanikiwa kwa ushirikiano wa wizara ya nishati na madini, mamlaka ya mapato na vyombo vingine vya ulinzi na sasa mzigo yatafanyika mahesabu tena Kujua thamani halisi ya Madini hayo)

Baada ya taarifa hizi Serikali iliamua kuunda timu ya Uchunguzi na hii ndio taarifa ya uchunguzi huo ikiwasilishwa na Prof. Mruma tena kwa Waziri wa Fedha

UPDATES:

Nimeikuta inaendelea katika television ya tbc 1

Hii kamati ya Uchunguzi iliiongozwa na Professor Mruma. Sasa ndo anatoa taarifa hiyo kwa Waziri wa Mipango na Fedha Dk. Mpango, Fuatilia matangazo hayo ya moja kwa moja.
Walisema thamani ya almasi iliyokamatwa ni Tsh 31.4bn ila kitaalamu Almasi ile ina thamani ya zaidi Tsh 64bn- Waziri wa Fedha, Dkt. Mpango

Wafanyakazi waliopita na waliopo katika ofisi ya Kamishna wa Madini wachunguzwe kufuatia wizi katika sekta ya madini- Waziri Mpango

Namtaka Gavana wa BoT aangalie upya suala la wao kuanza kuhifadhi madini ya vito. Haiwezekani kazi yao ikawa kuhifadhi fedha tu- Dk. Mpango

Prof. Mruma waambie wenzako wa Bodi ya Mwadui kwamba, mwaka huu serikali tunataka gawio na hatutaki makombo- Dkt. Mpango.

Wataalam wa tathmini ya madini ya vito waandaliwe, tuwe nao wa kutosha ndani ya miezi 6-7 na wapelekwe kwenye migodi haraka-Dkt. Mpango.

Waziri wa Fedha ameagiza upimaji wa madini uanzie mgodini na vifaa vinavyohitajika vinunuliwe mara moja.

Vyombo vya ulinzi na usalama lazima visimamie kikamilifu mali za watanzania. Vyombo hivyo visigeuzwe kuwa uchochoro wa kuiba- Dk Mpango.

Sasa timu nzima imeelekea sehemu ilipohifadhiwa na tayari wapo ktk chumba husika, protocol za kufungua chumba zinaendelea.

Sanduku lililohifadhi Almasi hiyo linafunguliwa sasa.

Prof. Mruma na watu wako mmefanya kazi ya kutukuka kwa Taifa na tumepokea mapendekezo yenu"-Waziri Dkt. Philip Mpango.

"Zilibaki dakika 5 tu ndege iondoke na kama si watendaji wazalendo tungeibiwa hizi almasi"-Waziri Dkt. Philip Mpango.

Vyombo vya dola nawataka muanzie migodini watu wote walioshiriki wachunguzwe na mbainishe mali zao"-Dkt. Philip Mpango

Nataka mapendekezo ya Prof. Mruma yafanyiwe kazi kwa 100%"-Waziri Dkt. Philip Mpango.

Upimaji wa Madini uanzie migodini na vifaa vya upimaji vinunuliwe mara moja"-Waziri Dkt. Philip Mpango.

"Lazima wawarudishie watanzania mali zao"-Waziri Dkt. Philip Mpango.

Wataalam wa tathmini ya madini ya vito waandaliwe, tuwe nao wa kutosha ndani ya miezi 6-7"-Waziri Dkt. Philip Mpango.

Prof. Mruma, waambie wenzako wa bodi ya mwadui, mwaka huu tunataka gawio na hatutaki makombo"-Waziri Dkt. Philip Mpango.
DJRWG-IXcAAeSnB.jpg
Waziri wa Fedha Dkt. Philip Mpango akioneshwa shehena ya mzigo wa almasi uliomatwa hivi karibuni Uwanja wa Ndege DSM.
mpango.PNG 
Kamishna wa Madini amesema itawachukulia hatua wote waliofanya uthaminishaji usio sahihi wa madini ya Almasi yaliyozuiwa kusafirishwa nje.

Waziri wa Fedha amemuagiza Kamishna wa Madini kutaifisha madini ya Almasi yaliyokamatwa kutokana na mgodi kudanganya juu ya thamani yake.

About Author Mohamed Abu 'l-Gharaniq

when an unknown printer took a galley of type and scrambled it to make a type specimen book. It has survived not only five centuries.

No comments:

Post a Comment

Start typing and press Enter to search