Amuua mpenziwe kwa ''mzaha'' katika YouTube
Amuua mpenziwe kwa ''mzaha'' katika YouTube
Mwanamke mmoja mjini Minesesotta
nchini Marekani amehukumiwa kwa kumpiga risasi na kumuua mpenzi wake
katika kile kinachosemekana ni mgogoro wa mtandaoni.Wawili hao wana mtoto wa miaka mitatu na takriban watu 30 walikuwa wakiangalia video hiyo ya YuTube alipompiga risasi mpenziwe.
Shangazie Ruiz anasema kuwa walifanya kitendo hicho ili kuimarisha ufuasi wao katika katika mitandao ya kijamii.
Claudia Ruiz aliambia runinga ya WDAY-TV kwamba binamu yake alimwambia kwamba alitaka kufanya kitendo hicho '' kwa sababu walihitaji kupata wafuasi zaidi''. ''tunataka kuwa maarufu''.
''Aliniambia kuhusu wazo hilo na nikamwambia'',''Musafanye hivyo''.
''Kwa nini utumie bunduki? Kwa nini?'', Claudia Ruiz aliambia chombo hicho cha habari.
''Walikuwa wakipendana sana'',alisema.''ulikuwa mzaha uliofanyika kimakosa''.
No comments:
Post a Comment